The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Suluhu Hassan Afanya Uteuzi

0

 

Rais Samia Suluhu Hassan, amewateua Mhandisi Rogatus Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi (Miundombinu), Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Tanroads na Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa pia Rais Samia amemteua Mhandisi Amin Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Tanroads, uteuzi ambao umeanza Juni 12, 2023.

 

Leave A Reply