The House of Favourite Newspapers

Rais Tshisekedi Awaonya Wakazi wa Goma

0

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amesema hali sio nzuri lakini ipo katika udhibiti baada ya kulipuka kwa volcano katika eneo Goma huko mashariki mwa taifa hilo.

 

Akizungumza baada ya serikali yake kutangaza kwa makosa kutokea mlipuko mwingine wa volkano, ikiwa ni takribani juma moja baada ya mlipuko wa Mlima Nyiragongo, Tshisekedi ameonya kwa kusema kwa hali ilivyo mlipuko unaweza kutokea kokote katika jiji la Goma kwa kuwataka wakazi wa mji huo kutoharakisha kurejea katika makazi yao.

Taarifa yake hiyo anaitoa baada ya kuwepo kwa ripoti zinazosema zaidi ya wakimbizi 1,000 wameondoka katika kambi walizokuwa wanahifadhiwa huko Rwanda kurejea Goma.

 

Takribani wakazi 400,000 waliokolewa katika eneo la mashariki la Goma, baada ya wiki moja ya matetemeko ya ardhi, yalitokana na mlipuko wa moja ya vokano hai barani Afrika.

 

Leave A Reply