The House of Favourite Newspapers

Rais Tshisekedi: Magufuli Mtetezi wa Kiuchumi Afrika

0

Rais wa DRC Felix Tshisekedi na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amesema DRC na Umoja wa Afrika kwa pamoja wamesikitishwa na kifo cha ‘mwanamapinduzi’ Dkt John Magufuli.

 

“Nina masikitiko makubwa yaliyojaa huzuni kwa kuondokewa na ndugu na rafiki yangu Magufuli. Msiba huu ni mzito, hauwagusi Watanzania pekee yake, kupotea na kuondoka kwa Dk Magufuli kumetingisha Bara la Afrika.

 

 

”Msiba huu si tu unagusa Watanzania pekee, bali kifo chake kimegusa bara zima la Afrika…bara la Afrika linajikuta yatima.. alilenga kuboresha maisha ya wananchi wake, pia aliyekuwa akitetea, kuendeleza uchumi kwenye bara letu la Afrika.

 

 

 

“Tutabaki na kumbukumbu, Magufuli alikuwa mpiganaji wetu na mzalendo wa kweli, sio tu kwa maslahi mapama ya watanzania bali ya Umoja wa Afrika, mtetezi wa uhuru wa bara la Afrika ambaye alikuwa analenga kutimiza ndoto za mshikamano za waasisi wetu wa bara la Afrika,” alisema Rais Tshsekedi.

 

 

Felix Tshsekedi amesema Hayati Magufuli alikuwa mtetezi mkuu wa uhuru wa kitamaduni na kiuchumi wa bara la Afrika, aliyekuwa akilenga kutimiza ndoto ya waasisi wa mataifa ya Afrika uliolenga kuleta umoja ndani ya bara hilo.

 

Leave A Reply