The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Nilipata Ugumu Kutangaza Kifo cha Magufuli – Video

0

Rais Samia Suluhu Hassan amesema alipata wakati mgumu sana kutangaza kifo cha mtangulizi wake John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam na kuwataka Watanzania kuamini kuwa kwa sasa yeye ndiye yupo katika usukani wa kuiendesha nchi.

 

 

Akizungumza leo wakati wa shughuli ya kitaifa ya kuaga mwili wa kiongozi huyo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Rais Samia amesema siku hiyo kuwa ngumu na leo ilikuwa siku ya pili kwa ugumu kwake anapotoa hotuba mbele ya jeneza lenye mwili wa mtangulizi wake.

 

 

“Nilipotakiwa kutangaza msiba wa Rais wangu nilipata wakati mgumu, nilijiuliza kama vile namkosea kiongozi wangu, lakini nikaambiwa mimi ndiyo natakiwa kufanya hivyo,” amesema Rais Samia.

 

 

Hata hivyo Rais Samia amesisitiza kuwa mtangulizi wake amemuachia mema yatakayokumbukwa wakati huu na vizazi vijavyo ikiwemo utendaji kazi wake ambao aliona muda wa saa 24 kwake haukuwa ukimtosha.

 

 

Bi.Samia amewataka Watanzania wenye mashaka watambue aliyesimama uwanjani hapo ni Rais licha ya kuwa yeye ni mwanamke. Amesema yuko imara kutokana na namna alivyolelewa na mtangulizi wake huyo kwa hiyo haoni kama kuna mahali watu wanaweza kuwa na hofu naye.

Leave A Reply