The House of Favourite Newspapers

Ramar Odom: Nammisi Sana Rob Kardashian

0
Lamar akiwa na Khloe

HUKU penzi lake na mtoto mkali kutoka katika familia ya kishua, Khloe Kardashian likiwa limekufa moja kwa moja, hatimaye aliyekuwa mcheza kikapu wa La Lakers, Odom Lamar amefunguka kwamba anamkumbuka sana shemeji yake, Rob Kardashian.

Akizungumza katika Kipindi cha The Wendy Williams Show, Lamar alisema wazi kwamba inawezekana kutofautiana na Rob ni kwa sababu alimuumiza mno dada yake huyo.

“Hatupo kama zamani, si yeye, hata kama ingekuwa kwangu, pia ningemkasirikia mtu ambaye amemuumiza dada yangu,” alisema Lamar huku akionekana kuumizwa na kilichokuwa kikiendelea.

Kwa sasa jamaa yupo poa baada ya kutoka rehab ambapo alikuwa akitibiwa tatizo lake la kutumia madawa ya kulevya huku Khloe akibanyuka na mcheza kikapu mwingine, Tristan Thomson.

 

Na: Nyemo Chilongani, (GPL)

Leave A Reply