The House of Favourite Newspapers

Tangalo Rasmi Miaka Miwili Namungo FC

0

 

FREDDY TANGALO, kiungo wa Lipuli, jana Jumatano, Agosti 5, 2020, amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Klabu ya Namungo FC ya Lindi.

Kiungo huyo amesaini dili hilo akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kwisha ndani ya  Lipuli yenye maskani yake Iringa na inayotumia uwanja wa Samora.

Huu ni usajili wa kwanza kwa Namungo FC ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery, ambaye anawania tuzo ya Kocha Bora kwa msimu wa 2019/20.

Lipuli msimu ujao wa 2020/21 itashiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushuka daraja msimu huu wa 2019/20 ikiwa nafasi ya 18 na pointi 44 baada ya kucheza mechi 38.

Namungo inaimarisha kikosi chake kwa sasa kwa ajili ya msimu ujao ambapo ina nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa ambapo itapeperusha bendera ya taifa ya  kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.

Nafasi hiyo wameipata baada ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho na kukutana na bingwa wa Ligi Kuu nchini, Simba SC, ambaye alishinda kwa mabao 2-1 Uwanja wa Nelson Mandela.

Licha ya kupoteza, Namungo imepata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa kuwa tayari Simba itaiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Leave A Reply