The House of Favourite Newspapers

Ray C apelekwa Sober kama Chid Benz

0

Ray-newRay C.

MWANADADA mkongwe kwenye tasnia ya Uimbaji mziki hapa nchini, Rehema Chalamila maarufu akam ‘Ray C’ jana Ijumaa alipelekwa kwenye kituo cha kinachosaidia watuwalioathirkia na utumiaji wa madawa ya kulevya kuachana nayo, kijulikanacho kama Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House) iliyopo Bagamoyo ambako miezi kadhaa iliyopita rapa Chid Benz alipelekwa kwa amatatizo kama hayo.

Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku moja toka Ray C aonekane katika video iliyosambaa mitandaoni ikionyesha jinsi alivyokuwa akisaidiwqa na jeshi lapolisi baada ya kudaiwa kutaka kijichoma kisu.

chid beenz (1)Chidi Benz

Mmoja kati ya wasimamizi wa kituo cha Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House) ambacho pia kilimsaidia Chidi Benz kuachana na matuzi ya Madawa ya kulevya, Karim Banji, amekili kumpokea Ray C kituoni hapo ili aanze kusaidiwa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.

“Kweli jana tumempokea Ray C, na kusema kweli kwa sasa siwezi zungumzia maendeleo yake kwa sababu ni siku ya kwanza, lakini leo mchana amekula vizuri na nimemuacha amepumzika,” alisema Karim.

Pia alisema bado hajajua Ray C atakaa kwa muda gani ndani ya sober house.

“Kusema kweli mgonjwa akiletwa hapa, atapimwa afya na baada ya hapo anawekwa katika chumba maalum kwa siku tatu ili aweze kukabiliana na hali ngumu, na baada ya hapo ataendelea na matibabu ya kawaida, kwa hiyo kikubwa ni kuombea tu,” alisema Karim.

Leave A Reply