The House of Favourite Newspapers

Rayuu airudisha ndoa yake

0

RAYUU

Na Hamida Hassan

Msanii wa Filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ ameirudisha ndoa yake iliyodaiwa kuvunjika siku chache baada ya kuolewa na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ahmedi Said.

Sosi aliyetoa habari hii alidai kuwa msanii huyo baada ya ukimya wa muda mrefu amefanyiwa pati ya kuagwa ‘send off’ juzikati ndani ya Ukumbi wa Green Light, Tabata jijini Dar huku akialika watu wachache.

“Juzi nilikuwa kwenye send off ya Rayuu, ndoa yake imerudi na amefanyiwa bonge la sherehe ingawa wasanii wenzake hawakualikwa, alikuwepo msanii mmoja anayeitwa Rose, zamani alikuwa akitumia jina la Rose wa Chuzi,” alisema sosi.
Ijumaa liliwasiliana na Rayuu na kumpa hongera zake kwa hatua hiyo ambapo alishukuru.

Leave A Reply