The House of Favourite Newspapers

Rayvanny Amzawadia Ndinga Mpya Director Wake

0

Msani Rayvanny kutoka WCB ameamua kuonyesha upendo kwa mtayarishaji wake wa video (director) Eris Mzava ama ‘China Boy’ kwa kumpa zawadi ya gari.

 

Rayvanny ameamua kumzawadia Eris Mzava gari aina ya Toyota Corolla Rumion, ikiwa ni jitihada za Director huyo katika kujituma na utendaji kazi wake na muda wa miaka mingi wakiwa bado pamoja.

 

Mzava ameonyesha kufurahishwa na zawadi hiyo, amemshukuru Rayvanny kadhalika na uongozi mzima wa Next Level Music (NLM).

 

Tukio hilo limejiri usiku wa kuamkia leo katika studio za Next Level Music ‘NLM’ zilizopo Mbezi Beach, jijini Dar es salaam. “NLM Big family @erismzava New 🚘” – ameandika Rayvanny kupitia ukurasa wake wa instagram.

Leave A Reply