The House of Favourite Newspapers

RC Makonda Akagua Ujenzi Wa Nyumba Za Magereza, Asifia (Picha +Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya Serikali ambapo ambapo mapema leo ametembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za askari katika Gereza la Ukonga na kukuta mradi unaendelea vizuri.

Akizungumza na mtandao wa Global Publishers, Makonda amesema kuwa anampongeza Brigedia Jenerali, Charles Mbunda ambaye ni msimamizi mkuu wa mradi wa Suma JKT  kwa kuwa ni mtu anayefanya kazi kwa bidii.

Alisema anawasihi watumishi wote wa serikali kuacha kupiga majungu kwani kazi zao ndizo zitawafanya wapande daraja.

 

“Mradi huu sasa umeenda vizuri kwa kuwa ulikuwa unasuasua, umeanza kujengwa baada ya Rais Magufuli kuona unasuasua akakabidhi kwa Suma JKT na sasa unaenda vizuri kwa kuwa yale aliyoyataka kuwa sasa hivi yanafanikiwa.

“Nampongeza msimamizi mkuu kwa  usimalizi na uzalendo wake na timu yake ninaamini miezi miwili na nusu ijayo majengo haya yatakuwa yamekabidhiwa kwa ajili ya matumizi ya askari wetu.”

 

Aidha, Makonda amemuomba Rais Magufuli kuwakabidhi jeshi hilo nyumba za NSSF zilizopo Tuangoma ili wajenge na yaweze kukamilika na watu kuishi.

“Naomba nianze na haya majengo ambayo yamekaa kwa muda mrefu, yalianza kujengwa 2004 mpaka leo hajakamilika kwa hiyo ninaweza nikampeleka Mh.Rais (Magufuli) ili aweze kuona zile nyumba ili tuweze kuwapatia jeshi hili ili liweze kukamilisha na watu waweze kuishi.

 

“Maana rasilimali inayopotea pale ni kubwa yanapokaa tu bila kumaliziwa na kwa kuwa kuna barabara nzuri, sisi ni rahisi kubadilisha ruti na daladala zikafika kule,”alisema.

(Stori: Neema Adrian, GPL)

Comments are closed.