The House of Favourite Newspapers

RC Mbeya Aunda Tume Kuchunguza Kifo cha Dereva

0

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ameunda tume ndogo ya watu wanne na kuipa jukumu la kuchunguza kifo cha dereva wa lori aliyefahamika kwa jina la Abdulhman Issa anayedaiwa kufia mikononi mwa polisi katika eneo la Shamwengo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

 

 

Chalamila amefikia hatua hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha askari polisi wakimshusha kwenye gari dereva huyo na hatimaye kubainika amefariki na mwili wake kuhifadhiwa katika hospitali ya Igawilo jijini Mbeya.

 

 

Akizungumza na wanahabari hii leo Chalamila amesema tume aliyoiunda itampa majibu ndani ya siku tatu kuanzia leo na endapo itabinika kuwa dereva huyo amefia kwenye mikono ya vyombo vya dola wahusika watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

 

 

Tukio hilo limetokea Januari 27, 2021, mwaka huu majira ya saa 12 jioni huku mkuu wa mkoa wa mkoa akizuia mwili wa marehemu kuzikwa hadi atakapopewa ripoti ya tume aliyoiunda.

 

Leave A Reply