The House of Favourite Newspapers

Rekodi Ya Yanga SC Yambeba Pluijm Singida

0
Kocha wa zamani wa Yanga, Hans van Der Pluijm.

KOCHA wa zamani wa Yanga, Hans van Der Pluijm, rekodi yake ya msimu uliopita akiwa na kikosi cha timu hiyo baada ya kucheza mechi tano, ameendelea kutembea nayo ndani ya timu yake mpya ya Singida United.

 

Kabla ya Pluijm kuondoka Yanga Novemba, mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na Mzambia, George Lwandamina, alikuwa kocha mkuu kisha Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi.

 

Kwa sasa Pluijm ni Kocha Mkuu wa Singida United inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 10 nyuma ya Simba, Mtibwa Sugar na Azam FC, huku ikiipita Yanga kwa nafasi mbili ambayo ina pointi tisa.

 

Akiwa Yanga msimu uliopita, Pluijm aliiongoza kucheza mechi tano za kwanza na kukusanya pointi 10 sawa na ilivyo msimu huu akiwa Singida United.

 

Mechi tano za msimu uliopita Yanga ilipata matokeo ya mabao 3-0 dhidi ya African Lyon, Ndanda 0-0 Yanga, Yanga 3-0 Majimaji, Mwadui 0-2 Yanga na Stand 1-0 Yanga.

 

Msimu huu, Singida United ilifungwa 2-1 dhidi ya Mwadui, Singida 2-1 Mbao, Stand 0-1 Singida, Singida 1-0 Kagera na Singida1-1 Azam.

Leave A Reply