The House of Favourite Newspapers

Rita Dominic wa Nollywood Zaidi ya Miaka 40 Bila Mtoto, Sasa Atamani Ujauzito

0

Rita-Dominic-11Nollywood:

MUIGIZAJI maarufu wa Nollywood, Rita Dominic alijikutwa kwenye wakati mgumu Jumapili iliyopita baada ya kuulizwa na mmoja wa mashabiki wake aliyetaka kufahamu endapo mwanadada huyo mwenye umri wa miaka zaidi ya 40 ana mtoto ama ana mpango wowote wa kuzaa hivi karibuni.

Shabiki huyo alikuwa ni miongoni mwa mashabiki wengi wa Rita Dominic aliokuwa akichati nao ‘live’ kwenye ukurasa wake wa Facebook wakiuliza maswali na yeye kuyajibu.

Rita aliamua kuchgua swali la shabiki huyo na kumjibu;

“Hapana, sina (anaamisha hana mtoto). Lakini natamani kuwa naye. Napenda sana watoto. ninahangaika kulifanyia kazi ili nizae.”

Aidh Rita hakusita kuelezea siri ya urembo wake alipoulizwa na shabiki wake.

Alisema:

“NHakunywa maji mengi sana, Nafanya sana kazi. Najitahidi kula vyakula sahihi ninapoweza,” alisema Rita.

Leave A Reply