The House of Favourite Newspapers

Road to Succes Yajipongeza Kufanikisha Kongamano la Wazungumzaji

0

Mzungumzaji wa mhamasishaji wa masuala ya mafanikio ya Kimaisha, Rodrick Nabe ametoa shukrani kwa jamaa na marafiki kwa kufanikisha kongamano za wazungumzaji lililofanyika Ukumbi wa City Mall Jijini Dar, Novemba 28 mwaka huu.

Katika kongamano hilo lililohudhuriwa na wasemaji  mbalimbali ndani na nje ya nchi mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Buchosa mkoani Mwanza, Mheshimwa Eric Shigongo ambaye naye alitoa somo kwa wageni waalikwa.

Kufuatia mafanikio makubwa ya kongamano hilo Mkurugenzi wa Taasisi ya Road to Succes, Rodrick Nabe waandaaji wa kongamano hilo walifanya hafla fupi ya kupongezana.

Mkurugenzi wa Global Group na Mbunge wa Buchosa mkoani Mwanza, Eric Shigongo akimpongeza Rodrick Nabe kwa kuandaaa kongamano hilo na kulifanikisha.  
Rodrick Nabe akimkabidhi keki, Shigongo baada ya kumshukuru kwa kumsaidia kufanikisha kongamano hilo.  
Meneja Mkuu wa Global Group (kulia) Abdallah Mrisho, akiwa na sehemu ya wageni wa heshima kwenye hafla hiyo.   
Hivi ndivyo keki ilikatwa.   
Eric Shigongo akimlisha keki Rodrick Nabe baada ya kumpongeza kwa kufanikisha kongamano hilo.   
Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho akimlisha keki, Dkt. Riziki Nkya kwenye hafla hiyo.   
Dkt. Riziki Nkya akimlisha keki Mhariri Mtendaji wa Global Group, Saleh Ally.  
Dkt. Riziki Nkya akifungua shampeni katika kuzidi kusherehesha tukio hilo.     HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL
Leave A Reply