The House of Favourite Newspapers

Robert Mugabe Ndiye Kiongozi Mzee Zaidi Duniani, Mzee Mwinyi ni wa 42 Waliostaafu

Rais Mugabe

Na WALUSANGA NDAKI| RISASI JUMAMOSI| NAJUA WAJUA, NAKUJUZA ZAIDI

KWA viongozi wazee zaidi duniani walioko madarakani, Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe, anaongoza orodha hiyo akiwa na umri wa miaka 93 na siku 12 leo, akiwa ameingia ikulu ya nchi hiyo akiwa waziri mkuu hadi sasa akiwa rais.

Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza

Anaye shika nafasi ya pili ni Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 1952 hadi leo ambapo atafikisha umri wa miaka 91 hapo Aprili 21, mwaka huu.

Beji Caid Essebsi

Beji Caid Essebsi, Rais wa Tunisia tangu mwaka 2014 hadi sasa, anashika nafasi ya tatu atakapofikisha miaka 91 ifikapo Novemba 29, akifuatiwa na Mwenyekiti  Halmashauri Kuu ya Bunge la Umma la Korea ya Kaskazini, Kim Yong-nam, mwenye miaka 90 na siku 25 ilipofika Februari 4, mwaka huu.

Kwa viongozi wazee zaidi waliopo madarakani na wale waliostaafu lakini wangali hai, Mugabe anashika nafasi ya 24, Elizabeth (53), Essebsi (62) na Kim (78).

Viongozi wazee zaidi waliowahi kushika madaraka lakini wangali hai, anayeongoza ni Do Muoi aliyekuwa waziri mkuu wa Vietnam tangu 1988 –hadi 1996, akawa pia Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunist tangu 1991 hadi 1997 akiwa na miaka 100 na siku 33 leo.

Huyo anafuatiwa na Babiker Awadall,  Waziri Mkuu wa Sudan tangu 1969 aliyefikisha miaka 100 Alhamisi iliyopita (juzi) ambapo anayeshika nafasi ya tatu ni Yasuhiro Nakasone aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan mwaka 1982 hadi 1987 atakayefikisha miaka 98 ifikapo Mei 27.

Mzee Mwinyi.

Kwa Afrika, Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa rais wa Tanzania tangu 1985 hadi 1995, anashika nafasi ya 42 duniani atakapokuwa na miaka 92 ifikapo Mei 8, mwaka huu ambapo aliyekuwa rais wa Zambia, Kenneth Kaunda tangu 1964 hadi 1991, anashika nafasi ya 32 duniani ambaye atakuwa na miaka 93 ifikapo Aprili 28, mwaka huu.

Rais Dawda Jawara wa Gambia

Rais Dawda Jawara wa Gambia aliyepinduliwa na Yahya Jammeh, anashika nafasi ya 33 duniani. Jawara alikuwa waziri mkuu wa nchi hiyo mwaka 1962 hadi 1970 na rais tangu 1970 hadi 1994 alipopinduliwa na Jammeh. Jawara atafikisha miaka 93 ifikapo Mei 16 akifuatiwa na aliyekuwa rais wa Kenya, Daniel arap Moi, tangu 1978 hadi 2002 atakayekuwa na miaka 93 ifikapo Septemba 2, mwaka huu.

Viongozi wengine wazee Afrika waliopo na waliwahi kushika madaraka ni aliyekuwa Waziri Mkuu wa Libya, Mustafa

 

(1954-57) ana miaka 96 na siku 34 leo (Jumamosi) akishika nafasi ya 16. Nafasi ya 17 inashikwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Katiba la Algeria, Abdelmalek Benhabyles mwaka 1992 akiwa na miaka 96 ifikapo Aprili 27.

Nafasi ya 41 duniani inashikiliwa na aliyekuwa rais wa Nigeria (1979-83) Shehu Shagari mwenye miaka 92 na siku 7 ilipofika Februari 25, mwaka huu akifuatiwa na Antoine Gizenga aliyekuwa Waziri Mkuu wa Congo-Kinshasa (2006-08) atakayefikisha miaka 92 ifikapo Oktoba 5 mwaka huu.

 

SHINDA NYUMBA AWAMU YA PILI YATIKISA JIJI LA DAR ES SALAAM

Comments are closed.