The House of Favourite Newspapers

Ronaldo Amkosha Mpenzi Wake Kwa Hoteli Baabkubwa

0

MPENZI wake staa anayesakata kabumbu katika klabu ya Juventus nchini Italia, Christiano Ronaldo, Georgina Rodriguez ameshindwa kuzuia furaha yake kutokana na juhudi za gwiji huyo baada ya kufungua hoteli mpya iliyopo katikati ya jiji la Madrid nchini Hispania.

 

Hoteli hiyo yenye thamani ya Euro milioni 13 sawa na Sh bilioni 37 ilipewa jina la Pestana CR7 Gran Via.

Kwa mujibu wa Ronaldo ambaye ni raia wa Ureno alisema hoteli hiyo ambayo ni ya tatu kwake, ilipangwa kufunguliwa Juni mwaka jana lakini ufunguzi huo ulisitishwa kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya Corona.

 

Katika uzinduzi huo alioufanya mwishoni mwa wiki, Ronaldo  alitoa ofa ya bei punguzo ya asilimia 41 kwa wasafiri watakaokuwa wanataka kulala katika hoteli hiyo yenye ghorofa 10 na vyumba vya kulala 168.

Aidha, kupitia akaunti yake ya Instagram, mpenzi wake Ronaldo alishusha ujumbe huu mwanana: “Hongera @cristiano kwa ufunguzi wa hoteli hii iliyobeba ndoto zako. Nimefurahiya sana hiki ulichokijenga tena kwa juhudi kubwa na ujasiri.

 

“Ninawaalika watu wote duniani waje kutembelea hoteli hii na kupata nafasi ya kipekee itakayosisimua maisha yao na kuwafanya wahisi kama wanaota.”

 Stori: Mushi Gabriel | GPL

Leave A Reply