The House of Favourite Newspapers

RONALDO ANUKIA UCHEZAJI BORA FIFA

0

 

RONALDO ANUKIA UCHEZAJI BORA
Christian Ronaldo.

RONALDO ANUKIA UCHEZAJI BORA…

Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji wanaowania Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), imeelezwa ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo. Ronaldo anayechezea Real Madrid alitwaa tuzo hiyo mwaka jana na mwaka huu akitwaa itakuwa ni mara yake ya pili mfululizo.

 

Tuzo hiyo inahusisha matukio ya wachezaji kati ya Novemba 20, 2016, hadi Julai 2, 2017, na mshindi huchaguliwa na makocha na manahodha wa timu za taifa, vyombo vya habari na mashabiki. Sherehe za tuzo hizo zitafanyika Oktoba 23, mwaka huu huko London. Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo kutokana na mafanikio aliyopata hivi karibuni.

 

Ronaldo aliisaidia Madrid kutwaa taji la tatu la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’, Kombe la Dunia la Klabu pia Kombe la Ulaya akiwa na Ureno.

 

Sambamba na Ronaldo, wengine wanaowania tuzo hiyo ni Lionel Messi wa Barcelona, Gianluigi Buffon wa Juventus, Toni Kroos, Luka Modric, Sergio Ramos, Marcelo, Neymar, Luis Suarez, Andres Iniesta na Alexis Sanchez wa Arsenal.

 

NA: MWANDISHI WETU| CHAMPIONI JUMAMOSI

Leave A Reply