The House of Favourite Newspapers

Ronaldo, Casemiro Waing’oa PSG Champions League

KLABU ya Real Madrid ya nchini Hispania imeing’oa timu Paris Saint German (PSG) ya Ufaransa wakiwa nyumbani baada ya kuichapa bao 2-1 usiku wa kuamkia leo.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kusisimua na wa aina yake, Madrid ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake nyota, Cristiano Ronaldo dakika ya 51 baada ya kumalizia kwa kichwa mkwaju wa Lucas Vazquez.

Dakika 20 baadaye, Edinson Cavani aliisawadhishia PSG dakika ya 71 ya mchezo huo.

Hata hivyo, Madrid waliongeza kasi zaidi hasa dakika 20 za mwisho hali iliyozaa bao la kuongoza dakika 80 baada ya Casemiro kufanya yake na kuiandikia Madrid bao la pili.

PSG wametolewa kwa jumla ya bao 5-2 baada ya kunyukwa bao bao 3-1 mechi ya kwanza iliyopigwa Madrid wiki mbili zilizopita.

Kukosekana kwa mshambuliaji wa Kimataifa wa PSG na timu ya Taifa ya Brazil, Neymar Jr, huenda ndiyo sababu iliyochangia vinara hao wa League 1 ya Ufaransa kuondolewa katika michuano hiyo ya UCL.

Katika game hiyo, Ronaldo amefikisha mabao 12 ya UCL kwa mwaka huu..

Kadi ya njano ya 33 kwa Sergio Ramos katika Champions League – idadi kubwa kuliko mchezaji yoyote katika historia ya michuano hii.

Paris Saint-Germain (4-3-3):

Areola 7; Alves 6, Marquinhos 5, Thiago Silva 6, Yuri Berchiche 6; Verratti 6, Motta 5, Rabiot 6; Di Maria 6 (Draxler 76), Cavani 6, Mbappe 6 (Diarra 86)

Subs not used: Trapp, Kimpembe, Lo Celso, Meunier

Manager: Unai Emery

Goals: Cavani 71

Yellow cards: Cavani 84

Red cards: Verratti 66

Real Madrid (4-4-2):

Navas 7; Carvajal 7, Ramos 7, Varane 7, Marcelo 6; Lucas Vazquez 8, Kovacic 8 (Kroos 72), Casemiro 7, Asensio 6 (Isco 82); Benzema 6 (Bale 76), Ronaldo 7

Subs not used: Casilla, Nacho, Hernandez, Modric

Manager: Zinedine Zidane

Goals: Ronaldo 51, Casemiro 80

Bookings: Kovacic 32, Ramos 78

SPOTI HAUSI: YANGA IKIFUNGWA INABAKI CAF, SIMBA BYEBYE!

Bao la Ronaldo dhidi ya PSG.

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Bao la ushindi la @casemiro #psg : 1 – 2 : #realmadrid ⚽ #UCL.

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Comments are closed.