The House of Favourite Newspapers

Ronaldo, Georgina Waanza Mwaka kwa Mahaba Mazito

0

SUPASTAA wa soka duniani, Cristiano Ronaldo na mchumba wake mrembo, Georgina Rodriguez, wameuanza mwaka kwa kuonyeshana mahaba mazito kwenye Mtandao wa Instagram.

 

Ronaldo, alianza kwa kumtumia ujumbe wa mwaka mpya mpenzi wake huyo ambaye ni muuza duka wa zamani, kisha naye akajibu.

Ronaldo aliandika: “Heri ya mwaka mpya, mpenzi wangu! 2020. Mwaka 2020 ujae mapenzi, afya, amani na mafanikio kwa wote! Heri ya mwaka mpya kwenu nyote!”

Georgina alijibu: “Kuhusu usiku uliopita…Uwe na 2020 ya furaha!!!! Afya zaidi na upendo kwa kila mtu.”

TURIN, Italia

Leave A Reply