The House of Favourite Newspapers

Rosa Ree Atoa Somo la Urembo

0

MREMBO anayefanya Hip Hop Bongo, Rasery Roberty ‘Rosa Ree’ amesema kuwa anajiamini kwamba yeye ni mzuri, ndio maana haoni sababu ya kupaka make up kila kukicha.

 

Akipiga stori na Risasi Vibes, Rosa Ree amesema kuwa wasichana wengi mjini ni wazuri, ila hawapendi kujiamini na kujikubali ndio maana mwisho wa siku wanadanganyika kwa vitu mbalimbali, maana wakisikia mtu anauza mafuta na kayafanyia promo ya kutosha atanunua, kesho akiona mengine mazuri zaidi ya yale aliyonunua atanunua tena.

 

“Niongee tu ukweli kutoka moyoni, mimi ni mzuri tena sana, namshukuru Mungu kwa hilo, halafu najiamini asikwambie mtu ndio maana mnaona hata make up huwa sipaki sana kwa sababu pia sizipendi. Hivyo, nawasihi na wasichana wenzangu wawe wanajiamini, wasipende kujaribu kila kitu, itawacost,” alisema Rosa Ree.

STORI: Memorise Richard, Risasi

Leave A Reply