Rose Ndauka Aipa Kisogo Sanaa!

MSANII aliyejipatia umaarufu kupitia tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amesema kuwa kwa hivi sasa ameipa kisogo sanaa, kwani anafanya biashara ya duka.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Kabula alisema kuwa, huko nyuma walikuwa hawajitambui ndio maana walikuwa wanakomaa na filamu pekee, lakini kwa sasa ni lazima kufanya kitu kingine nje ya sanaa ili kujiongezea kipato.

 

“Sasa hivi ndio mastaa wengine wanatambua kulikuwa na umuhimu wa kufanya vitu vingine nje ya sanaa, mimi sasa hivi nimeona sanaa iningoje kwanza maana kipaji ninacho lakini niuze duka langu, maana kwenye sanaa pesa ni ya kuingoja na hufanyi chochote,” alisema Kabula.

STORI | Imelda Mtema, Risasi


Toa comment