The House of Favourite Newspapers

RPC Shanna: Una UKIMWI, Hutaki Kupima, “You Are Going To Die Men!” – Video

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Jonathan Shanna amewataka askari wa jeshi hilo mkoani humo kuhakikisha wanapima afya zao ili kubaini iwapo wana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, waweze kujilinda na maambukizi ya ugonjwa huo hatari.

 

“Kwani ukipima Ukimwi kuna shida gani? Sasa wewe una Ukimwi halafu hautaki kupima, ‘you are going to die men, yes!’ (unakwenda kufa)…. Ukipima ukabainika unaanza kutumia dozi, unadunda tu, hata kama ukikutwa na tezi dume au kansa ya matiti kwa wanawake utatibiwa.

 

“Na uzuri ni kwamba, madaktari wetu ni wasiri mno, hawawezi kusema kwamba umeathirika, sasa wewe unaogopa nini? Ninaomba tupime afya,” alisema Shanna.

 

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIZUNGUMZA

Comments are closed.