The House of Favourite Newspapers

Rwanda Yamuachia Kagere kwa masharti

0

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere na kocha wa Namungo, Thiery Hitimana, leo Jumatatu wanatarajia kutoka nje ya makazi yao kwa mara ya kwanza baada ya Wizara ya Afya ya Rwanda kupunguza masharti ya katazo la kutoka nje ‘Lockdown’ kufuatia janga la virusi vya Corona.

 

Kagere na Hitimana walirejea nchini Rwanda kwa ajili ya mapumziko kufuatia ligi kusimama kutokana na ugonjwa wa Covid-19 unaosambazwa na Virusi vya Corona kabla ya nchi hiyo kuweka katazo la watu kutoka nje kwa kipindi cha siku 21 kutokana na ugonjwa huo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Hitimana alisema kuwa serikali ya nchi hiyo imepunguza masharti ya lockdown baada ya kuruhusu watu kurejea kwenye shughuli zao ikiwemo kutembea kuanzia leo Jumatatu.

 

“Binafsi hali bado siyo nzuri sana lakini jambo la kushukuru ni kwamba serikali imetoa ruhusa ya watu kuanza kutoka nje na kurejea katika shughuli zao za kila siku kwa sababu inaonekana huu ugonjwa siyo wa kuisha leo wala kesho.

 

“Lakini bado wameweka masharti kwamba hatuwezi kutoka nje ya mikoa zaidi ya kufanya shughuli katika maeneo ambayo watu wapo maana hata baadhi ya maeneo yanakutanisha watu wengi yataendelea kufungwa ikiwemo mipaka, safari za ndege hata safari za mikoani ila wangefungua na mipaka huenda ningeanza safari ya kurejea huko,” alisema Hitimana.

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

Leave A Reply