The House of Favourite Newspapers

Sallam Aibua utata kujitoa wasafi

0

DAR: Mmoja wa mameneja wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sallam Ahmed Sharaff ‘Mendez’ ameibua utata mpya wa kudaiwa kujitoa kwenye lebo hiyo ambayo inatajwa kuwa na mafanikio makubwa zaidi Bongo, IJUMAA WIKIENDA limekukusanyia habari kibindoni.

 

Hii sio mara ya kwanza kwa tetesi kuzagaa kuwa, meneja huyu amejitoa kwenye lebo hiyo, miezi kadhaa iliyopita, taarifa hizo zilisambaa na kulifikia gazeti hili lakini alipoulizwa Sallam, alichomoa.

 

Chanzo kilicho karibu na Wasafi kimeeleza kuwa, Sallam ameshajitoa kwenye lebo hiyo japo wenyewe wameamua kufanya siri ili kuepuka kuwavuruga mashabiki.

 

“Hawataki kuwachanganya mashabiki kwa habari hiyo ndio maana unaona wameamua kukaa kimya. Na hata ukiwauliza, wote watakwambia tu wapo sawa kumbe kiuhalisia hawako sawa, kila mtu ana maisha yake,” kilisema chanzo hicho.

 

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, Sallam kwa sasa yupo bize na miradi yake binafsi ikiwemo online televisheni pamoja na redio yake.

 

“Jamaa yupo bize sana na redio na televisheni yake. Kwa sasa hajishughulishi kabisa na ishu za Wasafi kwa sasa,” kilisema.

 

IJUMAA WIKIENDA lilifanya utafiti wake na kubaini kuwa siku za hivi karibuni, Sallam amekuwa haonekani kwenye matukio ya Wasafi ikiwemo lile muhimu lililowakusanya mameneja wote wa Mondi hivi karibuni.

 

Siku hiyo, Mondi alizungumza kupitia televisheni yake ya Wasafi ambapo walionekana pia mameneja wake, Said Fella na Hamisi Taletale ‘Babu Tale’.

 

Mameneja hao waliofika studio na kuonekana ‘live’, waliambatana na Mondi hadi kwenye hoteli mpya waliyoinunua iliyopo Mikocheni B jijini Dar ambako pia walizunguka kwenye jengo hilo na kufanya mahojiano, lakini Sallam hakuwepo.

 

Baada ya kujiridhisha na hayo, IJUMAA WIKIENDA lilimtafuta Sallam ambapo alipopatikana alisema kuwa, taarifa hizo zilianza kusambaa kwa muda mrefu lakini si za kweli.

 

“Mimi nashangaa hizi taarifa zinazosambaa kwenye mitandao sijui huwa wanazitoa wapi, nilianza kusikia tangu kipindi kile nipo Misri na bahati nzuri nilikuwa naye Mondi kwenye Caf.

 

“Sasa nikajua kuwa yameisha, lakini bado wanaendelea kusema kuwa nipo na Harmonize, siyo kweli mimi nipo bado Wasafi, na sitasita nikiwa nimetoka nitasema,” alisema Sallam.

 

Kutokana na majibu hayo, ukichanganya na utafiti uliofanywa na IJUMAA WIKIENDA, bado kuna utata ambao bado haujafunguka!

 

Majibu ya ukweli wa jambo hili yatakuja kuonekana siku za usoni. Iwe ni kumuona Sallam katika shughuli za Wasafi au kutomuona au yeye mwenyewe kutangaza kujitoa!

Leave A Reply