The House of Favourite Newspapers

Saby Angel: Afungukia Kufichwa Nje ya Nchi

0
Sabrinah Omary ‘Saby Angel’.

BAADA ya kupotea kwa kipindi kirefu huku tetesi zikienea kuwa amefichwa nje ya nchi na pedeshee, msanii wa filamu Bongo ambaye pia ni mwanamuziki, Sabrinah Omary ‘Saby Angel’ ameibuka na kufunguka kuwa hakufichwa bali alikuwa akifanya kazi zake binafsi.

 

Akizungumza na Star Mix, Saby alisema anashangazwa na wanaoendelea kuzusha vitu ambavyo hawavijui ukweli wake kwani vinamharibia sifa hata huko alipokuwa akifanya kazi. “Hii si mara ya kwanza kuzushiwa hayo mambo. Watu wa aina hii kiukweli wanakera sana tena zaidi ya sana.

 

Mimi kwa sasa nafanya zangu kazi binafsi, kuna wakati nipo Kenya, Dubai na nchi nyingine lakini siyo kwamba nimefichwa na mwanaume hataaa!” Alisema Saby.

Leave A Reply