The House of Favourite Newspapers

Sajent na Nisha wamgombea bwana

0

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Barakah Andrew ‘Barakah Da Prince’.

 

WAIGIZAJI wa fi lamu Bongo, Husna Iddi ‘Sajent’ na mwenzake Salima Jabu ‘Nisha’ wanadaiwa kuwa katika ugomvi mkubwa kumgombea msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Barakah Andrew ‘Barakah Da Prince’.

Salima Jabu ‘Nisha’

Chanzo makini kilicho karibu na wasanii hao kinasema Sajenti ndiye aliyeingilia kati penzi la wawili hao baada ya ujumbe wake wa simu kukutwa katika simu ya mkali huyo wa Bongo Fleva ambaye amekuwa katika uhusiano na Nisha kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
“Kuna siku Nisha alifuma meseji kwenye simu ya Barakah Da Prince ikiwa imetumwa na demu ambaye hakumfahamu mara moja, lakini baadaye akasikia kumbe ni Sajenti,” kilisema chanzo hicho.

Sajent-1.jpgHusna Iddi ‘Sajent’.

Barakah Da Prince alitafutwa na gazeti hili ili kuzungumzia madai hayo, lakini akashindwa kukubali wala kukanusha, alisema kwa sasa hayupo kimapenzi na Nisha kwa vile kwa zaidi ya wiki tatu kila mtu yupo kivyake baada ya kugombana.

“Dah, naomba nikutaarifu kuwa mimi siwezi kuwagombanisha maana tayari Nisha tumeachana tena kwa ugomvi mkubwa, ila hiyo ishu ya Sajent kiukweli nashindwa nikwambieje maana nakosa namna ya kukueleza ukaweza kunielewa hatua kwa hatua,” alisema. Kwa upande wake, Sajent alisema Barakah ni rafi ki yake tu, hivyo watu wakisema lao hawezi kuwazuia kwani wana uhuru wa kufi kiri na kuongea na kudai yeye siyo mtu wa kwanza kudaiwa kuingilia penzi la watu.

“Ifahamike kuwa kugombana kwao na Nisha mimi hakuwezi kunizuia kuishi maana Nisha si rafi ki yangu wala ndungu yangu, zaidi namjua kama msanii wa fi lamu tu na suala la yeye na Barakah mimi haliwezi kunipa shida yoyote ile, watu watakuwa wanajihisi na kutengeneza maneno, mimi siyo wa kwanza kusingiziwa jambo kama hili,” alisema Sajent. Nisha hakuweza kupatikana kupitia simu yake ya mkononi kwani muda wote ilikuwa imezimwa, hata alipotumiwa ujumbe kupitia Mtandao wa WhatsApp hakusema lolote juu ya ishu hiyo.

Leave A Reply