The House of Favourite Newspapers

Sajenti Adaiwa Kunasa Ujauzito wa Dullah Makabila

0
Msanii wa filamu za Kibongo, Husna Iddi `Sajenti’.

Dar es Salaam: Msanii wa filamu za Kibongo, Husna Iddi `Sajenti’ anadaiwa kunasa ujauzito wa staa wa Singeli Bongo, Dullah Makabila anayedaiwa amekuwa akitoka naye kimapenzi.

Staa wa Singeli Bongo, Dullah Makabila.

Chanzo chetu makini kiliiambia 3 Tamu kuwa, Sajenti ni mama kijacho na mhusika ni Dullah Makabila huku baadhi ya ndugu wa Sajent wakitambua ujio wa uzao huo.

3 Tamu ilimtafuta Dullah ambaye aliomba aachwe kwanza hadi pale atakapoweka wazi mwenyewe huku Sajent akifunguka: “Inawezekana ni kweli nina mimba, hata hivyo Dullah ni mwanaume aliyekamilika, sasa tatizo liko wapi?” Alihoji Sajenti.

Leave A Reply