Sajenti aumbuka

Sajent-1.jpgGladness Mallya na Hamida Hassan

KABANG! Baada ya kukataa kwa kipindi kirefu kuwa hajazaa, msanii asiyekuwa na bahati ya kutoka kisanaa, Husna Idd ‘Sajent’ hatimaye juzikati alinaswa live akiwa na mtoto wake wakati akimfanyia maulidi, Sinza Madukani jijini Dar es Salaam.

sajent (1) sajent (1)
Sherehe hiyo ya kumtoa mtoto ilifanyika nyumbani kwa dada yake, ambapo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali huku mwenyewe ‘akiwagwaya’ na kuwakataza baadhi ya waandishi kuingia kwa kinachodaiwa kuogopa sura ya mwanaye kuonekana gazetini.

sajent (2)Chanzo makini kilichokuwa ndani ya sherehe hiyo kilipenyeza habari na picha za mtoto huyo huku kikieleza kwamba anafanana kila kitu na anayetajwa kuwa baba yake mzazi, Gabo Zigamba ambaye pia ni msanii wa filamu.

“Yaani huyu mtoto anafanana kila kitu na Gabo, kwa mujibu wa mama yake aliwaambia baadhi ya marafiki zake kwamba mwanaume huyo alimkataa mtoto tangu akiwa tumboni na hamhudumii kwa lolote, hata kwenye sherehe hii hayupo.

sajent (3)“Unaambiwa hapa wanamsikitikia sana Sajent kwa sababu ni kama hana bahati kwani huyu ni mtoto wa pili, wa kwanza alizaa na mwanamuziki, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ ambaye kwa sasa ana familia yake na mtoto huyo anamlea peke yake,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta Gabo, mmoja kati ya waigizaji wanaofanya vizuri kwa sasa, lakini alishangazwa na taarifa hizo akidai hazitambui.

“Mimi sizijui hizo habari, kwanza nawashangaa nyie waandishi kuuliza skendo tu, kwa nini msiniulize kuhusu habari kubwa niliyonayo ya kwamba nawania tuzo nchini Nigeria, mmebaki kuniuliza tu ishu hizo, wewe ni mtu wa tatu sasa kuniuliza kuhusu hilo eti nilikuwa naishi naye Mwananyamala na kufunga naye ndoa ya siri, mlikuwepo?”

Kwa upande wake, Sajent aling’aka; “Hivi nilishawaambia huyu mtoto ni wa Gabo? Mtoto kufanana na Gabo siyo sababu kwani hata mimi nimefanana na watu ambao sijazaliwa nao kabisa na hii huwa inatokea kwa watu wengi sana duniani, naombeni mniache msinitafutie matatizo tafadhali.”


Loading...

Toa comment