The House of Favourite Newspapers

Samatta Aweka Rekodi ya Kibabe Wembley – Video

0

Mbwana Samatta amefunga bao lake la kwanza kwenye Uwanja wa Wembley kunako Dakika ya 41 wakati Aston Villa ikivaana na Manchester City katika fainali ya Kombe la Carabao.

 

Licha ya kufungwa bao 2-1 na Man City (Agüero 20′ Rodri Hernández 30′) ambao wamechukua kombe hilo usiku wa kuamkia leo, bao la Samatta lililoifutia machozi Aston Villa lilitosha kuwapa furaha Watazania na mashabiki na wahodha huyo wa Taifa Stars.

 

Samatta nanakuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika mchezo wa fainali dhidi ya Pep Guardiola tangu Wayne Rooney alipofanya hivyo mwaka 2011. Samatta anakuwa mchezaji wa tano Mwafrika kufunga bao katika fainali ya Carabao Cup baada ya Didier Drogba, Joseph-Désiré Job, Obafemi Martins na Yaya Toure

Pia anakuwa Mtanzania wa kwanza Kucheza Ligi Kuu ya Uingereza na kufunga bao, kucheza Klabu Bingwa Barani ulaya na kufunga bao. Kuwafunga Mabingwa watetezi (Liverpool – UCL) na Manchester City – EPL) mabao yote amefunga kwa kichwa.

 

Rekodi nyingine ambazo ameziweka siku za nyuma ni kushinda Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika akiwa na TP Mazembe,  kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Ubelgiji na kuchukua kombe la Ligi hiyo na nyingine kibao.

Villa mara ya mwisho kutwaa ubingwa ilikuwa msimu wa 1995/96 . Mechi ni Mapumziko; Manchester City inaongoza 2-1 dhidi ya Aston Villa.

Leave A Reply