The House of Favourite Newspapers

Samia: Huku Mna Kenyatta, Kule Kuna Suluhu, Kazi Kwenu! -Video

0

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya kushirikiana na si kushindana ili kuhakikisha uchumi wa mataifa hayo mawili unakua huku akitumia lugha ya utani, “Tanzania kuna Suluhu na Kenya kuna Uhuru.”

 

Ameeleza hayo leo Jumatano Mei 5, 2021 katika kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya linalofanyika Nairobi nchini Kenya ambapo pia lilihudhuriwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

 

Samia amesema kuingia kwenye ushindani usio na tija hauwezi kuwa na matokeo chanya katika mataifa hayo mawili na kutaka ushirikiano kuwa kitu cha mbele zaidi.

 

“Mna bahati kwamba nchi zetu mbili upande mmoja kuna Uhuru wa kufanya biashara na upande mwingine kuna Suluhu ya kuondoa vikwazo vya kuendesha biashara kwa hiyo sasa mshindwe nyinyi,” amesema huku akitabasamu na kuwafanya washiriki wa kongamano hilo kucheka.

 

“Tanzania ipo tayari kuwapokea wafanyabiashara kutokana Tanzania, milango yetu ipo wazi na mikono yetu iko tayari kuwakumbatia. Serikali yangu ipo tayari kuwa daraja katika kuhakikisha biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi unafanikiwa.”

 

Awali Rais Kenyata alieleza kuwa ana matumaini makubwa kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia.

 

Leave A Reply