The House of Favourite Newspapers

Sanchi Abadili Dini

0

Mwanadada mwenye figa matata Bongo, Janey Rimoy maarufu mtandaoni kwa jina la Sanchi au Sanchoka amerejea katika vichwa vya habari, safari hii ikiwa ni kutokana na hatua yake ya kuamua kubadili dini na kuwa Muislamu.

 

Sanchi ambaye hivi sasa jina lake ni ‘Surraiya‘ ameandika habari hizo kwa mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram akitoboa siri ya kilichomsukuma kubadili dini na kuwa Muislamu.

 

Sanchi aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia mitandaoni, ameeleza furaha aliyonayo hivi sasa baada ya kusilimu Ijumaa (24/04) huku akitoboa siri kuwa amekuwa akifunga Ramadhani tatu mfululizo kwa kuwa alikuwa anaipenda dini ya Uislamu, lakini mara hii imekuwa ya kipekee kwani yupo ndani ya mfungo wa Ramadhani akiwa Muislam kamili.

 

Aidha, Sanchi amewatakia Waislamu wote mfungo mwema ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

 

“ALHAMDULLILAH moyo wangu una amani kupita nitakavyoweza kuelezea na ALLAH shahidi 😭 It’s official my spirit is where it truly belongs… Najivunia kufanya shahada yangu jana.. 24/04 Call me SURRAIYA EVARIST RIMOY.

 

Nimekua nikifunga Ramadan tatu mfululizo just because i love Islam but this one is very special, this is my first Ramadan as a Muslimah 🙏🏽🙏🏽 Alhamdullilah kwa hili na mengine mazuri yajayo INSHA’ALLAH.

Nawatakieni waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu.
Wabillahi Taufiq Walhidayah, Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh. 🤲🏽❤️” SANCHI

Leave A Reply