The House of Favourite Newspapers

SATF Yawakutanisha Wanufaika wa Vyuo 2021/22

0

Shirika la Social Action Trust Fund ( SATF ) ambalo limekuwa likitoa msaada kwa Watoto wenye uhitaji kufikia malengo yao kwa kuhakikisha wanapata mahitaji ya msingi kama vile elimu bora na afya, wamefanya kongamano na wanafunzi waliofaulu na kujiunga na elimu ya vyuo kwa mwaka wa masomo 2021/2022 ambao wamekuwa wakipatiwa msaada na shirika hilo.

Kongamano hilo lililofanyika Disemba 02, 2022 katika Hotel ya Mbezi Garden Jijini Dar es saalam limehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SATF Ms. Beatrice Mgaya, viongozi mbalimbali wa SATF pamoja na Mwandishi wa vitabu na Muhamasishaji maarufu nchini Joel Nanauka, ambapo wanafunzi wamepata nafasi ya kujifunza elimu ya kijinsia, maambukizi ya UKIMWI na ujuzi mbalimbali wa kimaisha.
Sambamba na hilo SATF limetoa zawadi mbalimbali zikiwemo tuzo na pesa taslimu kwa wanafunzi waliopata ufaulu mzuri na kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Leave A Reply