The House of Favourite Newspapers

Savio, DB Lioness Wachota Mil 15 Za NMB

Septemba 11, 2018 ilikuwa siku ya neema kwa timu za Kikapu za Savio na DB Queens zinazolelewa na Kituo cha michezo cha Don Bosco baada ya kupata udhamini wa vifaa kutoka kwa Benki ya NMB.

 

Timu hizo zimepata udhamini huo ukiwa ni wa vifaa mbalimbali vya kuchezea ambavyo viligharimu kiasi cha milioni 15.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Don Bosco, Upanga jijini Dar, Meneja Mwandamizi wa wateja Binafsi wa NMB, Ally Mngingite amesema wametoa udhamini huo kwa timu hizo mbili ikiwa ni baada ya kuombwa kuzidhamini wakati huu wakiwa wanajiandaa na mashindano ya mchezo huo wa kikapu.

 

“Udhamini huu wa vifaa vya michezo ni sehemu ambayo wao waliomba kwa ajili ya kuwadhamini. Hii ni sehemu ya fungu letu ambalo tumetenga kwa ajili ya kusaidia michezo.

“Fungu hilo linafika hadi bilioni moja ambazo tumeweka kwa ajili ya kusaidia michezo mbalimbali nje na huu wa kikapu ambao tumewadhamini leo (jana),” alisema Mngingite.

 

Naye Rais wa Chama cha Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa amesema: “Ninawapongeza kwa kuzidhamini timu hizi lakini niwaambie kama itawezekana mzidhamini na timu nyingine zinazoshiriki mchezo huu wa kikapu.

Comments are closed.