The House of Favourite Newspapers

Semina ya Mabadiliko ya Simba SC Yaanza

0
Ratiba ya semina hiyo.
Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam leo imeanza rasmi semina maalum kwa wanachama wa klabu hiyo ikiwa ni kutoa mafunzo ya mambo mbalimbali yanayoihusu Simba.
Wanachama wakimsikiliza Haji Manara akitoa mada.

TAZAMA Muundo Mpya wa Klabu ya Simba na Mabadiliko ya Katiba

Semina hiyo imejikita katika kuwajengea wanachama wake uelewa mpana zaidi juu ya muundo mpya wa klabu, uliotokana na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa na wanachama hao na kusajiliwa na Msajili wa Vilabu nchini.
Manara akifafanua jambo.
Wanachama wa Simba wamejitokeza kwa wingi kwenye Ukumbi wa Mikumi uliopo kwenye eneo la Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba (PTA), Kurasini jijini Dar es Salaam ili kuhudhuria semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Baadhi ya viongozi wa Simba waliojitokeza kutoa mada katika semina hiyo ni pamoja na msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara na Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Mzee Hassan Dalali.
NA MUSA MATEJA | GPL

TAZAMA Mapokezi ya Azam FC Himid Mao Afunguka

Leave A Reply