The House of Favourite Newspapers

Serengeti Boys Kuivaa Mali Leo

0

STORI: Ibrahim Mressy | CHAMPIONI| Dar es Salaam

TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa Miaka 17, Serengeti Boys, leo Jumatatu inafungua pazia lake katika mashindano ya Kombe la Afrika kwa Vijana, kwa kumenyana na Mali katika michuano hiyo inayofanyika nchini Gabon.

Serengeti Boys ipo Kundi B, pamoja na timu nyingine za Angola na Niger ambazo nazo zitakuwa kibaruani leo.

Akizungumza na Champion Jumatatu kwa njia ya simu jana, kocha mkuu wa kikosi hicho, Bakari Shime, alisema kuwa kikosi chake kipo vizuri na kimejiandaa vya kutosha kuwakabili vijana wa Mali kwenye mchezo huo wa kwanza.

“Kikosi kipo vizuri na tumejipanga kuikabili vilivyo timu ya Mali kwani tunataka kuwafurahisha Watanzania kwa kutowaangusha na naomba wazidi kutuombea,” alisema Bakari Shime.

Baada ya mchezo wa leo Jumatatu, Serengeti itakuwa kibaruani tena Alhamisi hii itakapovaana na Angola.

Yanga haishikiki kwenye mbio za Ubingwa

Leave A Reply