The House of Favourite Newspapers

Serengeti Boys Ni Mashujaa, Huu Usiwe Mwisho Wao

0

Bodi ya Uhariri | CHAMPIONI| Maoni

JUZI Jumatano, kikosi cha Serengeti Boys, kiliwasili jijini Dar es Salaam kikitokea Gabon kilipoenda kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri huo.

Michuano hiyo ambayo tamati yake inatarajiwa kuwa keshokutwa Jumapili, Serengeti iliishia hatua ya makundi baada ya kufungwa mchezo wake wa mwisho dhidi ya Niger, Jumapili iliyopita. Matokeo ya kuondoshwa kwa timu hiyo yamepokelewa masikitiko na Watanzania wengi waliokuwa wakiisapoti.

 Championi tunatoa pongezi kwa vijana wetu hao kwa kiwango walichokuwa wakikionyesha tangu katika mechi za kufuzu, za kirafi ki na zile za mashindano yenyewe ambapo walishinda moja, sare moja na kupoteza moja.

Kwa kiwango walichokionyesha Serengeti Boys, ni dhahiri kwamba Tanzania tukiamua kuiandaa timu vizuri basi matumaini ya kufika mbali yanakuwepo.

Hivyo basi, kutokana na hali hiyo, kikosi hicho kinatakiwa kutunzwa ili siku za baadaye wachezaji hao ndiyo waje kuitumikia timu ya wakubwa, Taifa Stars.

Mifano ya wazi ipo mingi ambapo timu inafanya vizuri, ukipita muda kidogo inatelekezwa na wachezaji wake kusambaratika na kupoteza ndoto zao.

Waandaliwe vema vijana wengine watakaorithi mikoba yao kwa sababu tunafahamu kwamba michuano ijayo ya vijana wenye umri huo itafanyika hapa kwetu mwaka 2019.

Leave A Reply