The House of Favourite Newspapers

Serengeti: Ngariba Nguli Atupwa Jela Miaka 5

0

NGARIBA nguli Mary Onyango Omega (50) maarufu Mkungu Mugesi mkazi wa kijiji cha Kitarungu Kata ya Nyansurura amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara miaka mitano jela kwa kosa la kumfanyia ukatili mtoto (ukeketaji).

 

Adhabu hiyo ni ya pili kutolewa na Mahakama tofauti ambapo Aprili 28,2021 katika kesi ya Jinai 151/2020 yeye na mzazi wa mtoto aliyefanyiwa ukatili mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Ismael Ngaile walihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini ya Sh 500,000 na kumlipa fidia ya Sh 1,000,000 mtoto aliyefanyiwa ukeketaji,alitoka gerezani baada ya kulipa.

 

Katika kesi ya Jinai namba 157/2020 mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Serengeti Judith Semkiwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela bila faini kwa kosa la kumfanyia ukatili(ukeketaji)mtoto mwingine tofauti na kesi ya awali ,hata hivyo ngariba huyo hakuwepo mahakamani wakati adhabu hiyo inasomwa.

 

Mwendesha mashitaka wa Jamhuri Faru Mayengela amesema mshitakiwa alikamatwa aprili 11,2020 katika kijiji cha Kitarungu akikabiliwa na makosa ya kuwafanyia watoto ukatili,ambao katika gwaride maalum la utambuzi walimtambua bila mashaka yoyote.

Leave A Reply