The House of Favourite Newspapers

Serikali: Mwisho Wa Namba Za 3d Kwenye Magari Ni Machi 15, 2024

0

Serikali imetoa siku 14 kuondolewa kwa namba za Magari zilizoongezwa ukubwa (3D), Vimulimuli kwa Magari yote yasiyoruhusiwa kuwekwa, namba zenye vibao vyeusi na zinazotumia namba za chasis, taa na stika ambazo zimeongezwa kwa matakwa ya Wamiliki au Madereva

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Jumanne Sagini amesema namba hizo hazitengenezwi na Wakala aliyepata kibali kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na pia herufi hizo zina ugumu wa kusomeka katika umbali usiopungua Mita 100

Naye, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Ramadhani Ng’anzi amesema Kiusalama Namba za 3D sio salama na Namba za Magari lazima ziwe 2D kutokana na Mifumo na Kamera kutotambua 3D

Leave A Reply