The House of Favourite Newspapers

Serikali Yaingilia Ujenzi Uwanja wa Yanga

0

 

SERIKALI imeipiga ‘stop’ Yanga kuendelea na ujenzi wa uwanja wao wa mazoezi eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam yalipo makao makuu ya klabu hiyo, kufuatia eneo hilo kuwa katika mchakato wa kurekebishwa kutokana na kuathiriwa na mafuriko ya mara kwa mara wakati wa mvua.

 

Zaidi ya miaka miwili sasa, Yanga wamekuwa wakikusanya vifusi na kuvimwaga kwenye eneo lao la uwanja ili kuhakikisha wanaliinua tayari kwa kuanza ujenzi wa uwanja huo jambo ambalo limeonekana kuwa gumu sasa kufuatia serikali kuwazuia hadi pale michoro itakapokamilika.

 

Mwenyekiti wa Yanga, Dkt Mshindo Msolla, amesema walitarajiwa kukamilisha uwanja huo ifi kapo Januari, mwakani jambo ambalo kwa sasa limeshindikana kutokana na hatua hiyo ya serikali.

 

“Kamati yetu ya ujenzi imeshindwa kuendelea na sakata la ujenzi wa uwanja wetu wa Jangwani na badala yake sasa tumeanza rasmi kujenga kule Kigamboni ambako tulipatiwa na RC Makonda (Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda), maana hatuna ujanja mwingine wa kuhakikisha tunatekeleza suala hili mapema kama tutaendelea kusubiria michoro ya serikali.

 

“Harakati za ujenzi wa Kigamboni zimeshaanza kwa kufyeka miti yote na ndani ya wiki mbili zijazo kamati itaanza kutifua eneo lote la uwanja kisha watatembelea viwanja mbalimbali vinavyoendelea kujengwa nchini ili kupata uzoefu na mbinu za kisasa zaidi, hatimaye ujenzi utaendelea,” alisema Msolla.

Musa Mateja, Dar es Salaam

Leave A Reply