The House of Favourite Newspapers

Serikali Yakabidhi Magari ya Mradi wa REGROW Mkoani Morogoro

0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiongea leo kwenye hafla ya kukabidhi magari hayo iliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

 

Amesema, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatekeleza mradi wa kukuza utalii kusini mwa Tanzania (REGROW) ambapo itakabidhi malori 44 yenye thamani ya shilingi bilioni 14.77 kwa TANAPA ambayo yatasambazwa katika hifadhi 4 za kusini ambazo ni Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa, Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (eneo lililojulikana kama pori la akiba la Selous).

 

Magari yaliyokabidhiwa kwa TANAPA

“Malori hayo pamoja na mitambo 18 ambayo ilishakabidhia hapo awali yataimarisha uwezo wa TANAPA kutengeneza barabara na viwanja vya ndege kwaajili ya matumizi ya watalii lakini pia kuongeza uwezo wa kufanya doria na kulinda maliasili zetu katika hifadhi za kusini” alisema Mpango.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango akiwasili kwa ajili ya hafla ya kukabidhi magari kwa TANAPA

Pia amewahasa watumishi wa tanapa watakao kabidhiwa magari hayo kuyatunza vizuri na kuyatumia matumizi yalio sahihi. Aliendelea kwa kusema kuwa mradi wa Regrow unatekelezwa na fedha za mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya dunia “Huu ni mkopo, mkopo ambao utalipwa kwa jasho la Watanzania kwahiyo wizara nayo ihakikishe vifaa hivi vinafanya kazi iliyokusudiwa na sio vinginevyo”

 

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply