The House of Favourite Newspapers

Corona: Serikali Yaongeza Mishahara, Hakuna Kulipia Maji

0

RAIS wa Ghana, Nana Addo Dankwa Akufo-Addo, ametangaza kuwalipia wananchi ankara za maji kwa miezi mitatu (Aprili, Mei na Juni), kutokana na watu kutoruhusiwa kutoka nje. Aidha, watumishi wa afya hawatolipa kodi katika miezi hiyo, na watapewa nyongeza ya 50% ya mishahara yao katika kipindi cha mwezi Machi hadi Juni 2020.

 

Amesema hatua hiyo ni katika kuimarisha vita dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 unaoambukiza kutokana na virusi vya Corona, ambapo pameanzishwa mfuko maalum utakaosimamiwa na Jaji Mkuu mstaafu, Sophia Akuffo.

 

Kwa mujibu wa  Akufo-Addo, srikali pia inatayarisha wafanyaakazi 1,000 wa tiba na 1,000 wenye kujitolea kusaidia kuwapata watu walioshirikiana na watu walioambukizwa.

 

Pia ametangaza mpango utakaogharimu GHC bilioni 1 za Ghana utakaochochea uchumi wa nchi hiyo ambao umedorora kutokana na shambulio la ugonjwa huo.

 

Vilevile, amesema watu 78 waliokuwa wamewekwa karantini wakati wa kuanza kwa shambulio la virusi hivyo, waligundulika kuwa na ugonjwa huo.  Amesema pia kwamba asilimia 97 ya matukio ya ugonjwa huo yameletwa nchini humo kutoka nje.

 

Rais Nana Addo Dankwa Akufo-Addo

 

 

 

Leave A Reply