The House of Favourite Newspapers

Serikali Yapendekeza Kuanzishwa Kwa Bima ya Afya kwa Wote – Video

0

DODOMA; Serikali inapendekeza kuanzishwa kwa mfuko wenye lengo la kugharamikia Bima ya Afya kwa Wote wasio na uwezo, aidha mfuko utaweza kutumika kugharamia huduma za matibabu kwa magonjwa sugu na ya muda mrefu kama vile saratani na magonjwa ya figo na huduma za dharura zitokanazo na ajali.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo Novemba 1, wakati wa kikao cha Bunge Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote wa mwaka 2022.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imepokea malalamiko mengi kuhusu watu wenye changamoto ya magonjwa ya figo na saratani na hivyo kushindwa kupata huduma za matiubabu kwa sababu ya kukosa fedha na kuongeza kuwa serikali imewasikiliza Watanzania hivyo itagharamia sehemu ya matibabu kwa magonjwa sugu na yale ya muda mrefu na hivyo Bima ya Afya kwa Wote ni mkombozia wa afya za Watanzania.

Leave A Reply