The House of Favourite Newspapers

Shambulio Laua 5 Nje ya Hoteli Somalia

0

3804-somaliacarbomb

WATU watano wameuwa katika shambulio la bomu lililotokea leo nje ya hoteli moja ya kitalii katikati ya Mji wa Mogadishu nchini Somalia karibu na lango la jumba la rais.

Lori lililokuwa na mabomu lililipuka nje ya hoteli hiyo iitwayo Somali Youth League (SYL). Kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab limekiri kutekeleza shambulio hilo.

Mtu mmoja aliyeshuhudia mlipuko huo amesema kuwa ameona watu wengi wakiwa wamejeruhiwa. Amesema kuwa hoteli hiyo imeharibika vibaya na kwamba vikosi vya usalama vimewasili katika eneo hilo.

Somali government soldiers and African Union Mission in Somalia (AMISOM) peacekeepers secure the scene of a suicide car explosion in front of the SYL hotel in the capital Mogadishu January 22, 2015. The Somali Islamist group al Shabaab claimed responsibility for a bomb attack at the gate of the hotel where Turkish delegates were meeting on Thursday, a day ahead of a visit by their president, Tayyip Erdogan, to the Somali capital. REUTERS/Feisal Omar (SOMALIA - Tags: CIVIL UNREST POLITICS CRIME LAW MILITARY)

Vyombo vya habari vinasema kuwa mkutano wa usalama ulitarajiwa kufanyika katika hoteli hiyo ya SYL.
Hoteli hiyo imeshambuliwa mara kadhaa na Al-Shabaab katika miaka ya hivi karibuni.

Leave A Reply