The House of Favourite Newspapers

Shamsa Ford: Ulikuwa Mfungo Wangu Halali

0

 

STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliomalizika, ulikuwa ndiyo mfungo wake halali kuliko yote aliyopita, kwani alifanya hivyo akiwa katika ndoa.

 

Akipiga stori na Za Motomoto News, Shamsa alisema mwaka huu amefunga kihalali mwezi mzima tofauti na miaka iliyopita ambayo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume Mkristo ambaye wakati mwingine alitaka kuwa naye bila kujali mfungo.

 

 

“Mwaka huu nimefunga na kumaliza Ramadhani kihalali maana niko ndani ya ndoa siyo kama miaka iliyopita nilikuwa nafunga kama mchezo, kiukweli najivunia sana kumaliza salama mwezi huu, natamani ungeendelea maana ulikuwa wa utulivu hivyo nawasihi wasanii wenzangu tuendelee hivihivi pia kujisitiri kama tulivyokuwa tunajisitiri kwa nguo za heshima,” alisema Shamsa.

Leave A Reply