Shein Asema Uchumi wa Zanzibar Umeimarika, Atangaza Elimu Bure

Sherehe za mapinduzi  Shein atangaza elimu bure.

Rais   wa Serikali ya Mapindizu ya Zanzibar  Dkt. Shein ametangaza kutoa elimu ya Sekondari bure katika sherehe za maadhimisho  ya  miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo  zimefanyika leo Januari 12, 2018 katika Uwanja wa Amani, Visiwani Zanzibar, ambapo viongozi wakuu wa nchi walihudhuria pamoja na mamia ya wananchi.

 

Dkt. Shein aliongoza sherehe hizo ikiwemo kukagua gwaride maalumu lililoandaliwa ambapo ametangaza rasmi kuwa serikali yake itaanza tena kutoa elimu ya sekondari bure kuanzia mwezi Julai mwaka huu huku akiwataka wananchi kuunga mkono juhudi za serikali za kuwaletea maendelo thabiti wananchi wake

 

Alisema kuwa Serikali zote saba ambazo zimehudumu baada ya mapinduzi zimefanya mengi ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari katika mwaka 2017 ambapo mapato yameongezeka kwa shilingi bilioni 61.097 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2016 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 12.5.

 

“Kasi ya ukuaji wa uchumi wetu imeongezeka kwa asilimia saba kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka 2016, pato la mtu binafsi limeongezeka kufikia Sh. 1,806,000 ikilinganishwa na Sh. 1,632,000. Idadi ya watalii visiwani Zanzibar imeongezeka kwa asilimia 14.2 kutoka watalii 379,242 mwaka 2016 hadi kufikia watalii 433,116 mwaka 2017.”

 

Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na wengine.

Na Mwandishi wetu

 

VIDEO: MSIKILIZE HAPA AKIZUNGUMZA

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment