The House of Favourite Newspapers

Shigongo Achimba Visima vya Maji Buchosa

0

 

IKIWA ni mkakati kuhakikisha tatizo la maji linamalizika katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Buchosa, Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Eric Shigongo kwa kushirikiana na wizara ya maji wameanza zoezi la kuchimba visima virefu vya maji katika maeneo ambayo yanashida kubwa ya huduma ya maji Jimbo hilo.

 

 

Zoezi Hilo limeanza katika Kijiji cha Chema kata ya Bupandwa Halmashauri ya Buchosa ambapo kisima hicho kinatarajia kuhudumia wakazi wa vitongoji vya Nyashimba B na Chema katika kata ya Bupandwa.

 

Baadhi ya wananchi wa vitongoji hivyo wamesema uchimbaji wa kisima hicho karibu na maeneo yao kutawasaidia kupunguza changamoto ya kufuata maji umbali mrefu ambao ulikuwa unasababisha wanafunzi kupata ujauzito na baadhi ya wanandoa kufarakana kutokana na wanawake kutoka ndani nyakati za usiku kwenda kufuata maji huku waume zao wakihisi wanawasaliti.

 

“Yaani Tunamshukuru Sana Mbunge wetu, Eric Shigongo pamoja na wizara ya maji kwa kutuletea kisima hiki kutapunguza adha tuliyokuwa tunapata ya kufuata maji umbali mrefu na tutalinda ndoa zetu!” wamesema wananchi hao.

Leave A Reply