The House of Favourite Newspapers

Shigongo Apokea Mabomba Mradi wa Maji Buchosa – Video

0

MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, amepokea mabomba 300 awamu ya kwanza kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji kutoka Nyehunge kwenda Hospitali ya Wilaya Isaka na vijiji jirani ambapo mradi huo utapita.

 

Shigongo amesema Jimbo la Buchosa linakabiliwa na upungufu mkubwa wa maji lakini kutokana na juhudi ambazo wameendelea kuzifanya kwa kushirikiana na ofisi ya Ruwasa Wilaya ya Sengerema anaamini tatizo la maji katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo yatamalizika.

 

“Mimi kama mbunge wa Buchosa, nitasimamia ipasavyo  ili mradi huu muhimu kwa wananchi wetu uweze kukamilika kwa wakati na wananchi wapate maji safi na salama.

 

“Mradi huu pia utapunguza kwa kiasi kikubwa  adha kwa wananchi kukosa maji na kupunguza vifo vya watu wanaoliwa na mamba kwenye ziwa pindi wakienda kuchota maji,” amesema.

 

NA IDD MUMBA | MWANZA

 

Leave A Reply