The House of Favourite Newspapers

Shigongo Apokea Vitanda vya Wagonjwa Buchosa – Video

0

MBUNGE  wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, amepokea vitanda vitano kutoka Hospital ya Tanzanite iliyoko Iseni jijini Mwanza kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kome ambacho kina upungufu mkubwa wa vitanda vya kulalia wagonjwa.

Shigongo amesema serikali inafanya mambo mengi sana katika Jimbo la Buchosa lakini haiwezi kufanya kila kitu, hivyo inahitajika wadau wa maendeleo kuisapoti.

“Hospitali ya Tanzanite imefanya jambo kubwa na la kiutu la kuisapoti serikali na kuwasaidia wananchi wa jimbo langu la Buchosa.

“Mimi niwaombe tu watu wenye nafasi ya kuchangia maendeleo waendelee kujitokeza kuisaidia serikali yetu na kuwaletea maendeleo wananchi wetu,” amesema Shigongo.

 

Leave A Reply