The House of Favourite Newspapers

Shigongo Anaendelea Kugawa Vifaa vya Shule kwa Wanafunzi

0

OFISI ya Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, imeendelea na zoezi la kugawa sare na madaftari kwa wanafunzi wa shule za msingi katika kata za jimbo hilo ambapo kata ya Kalebezo na Luhoranyonga zimefikiwa huku wazazi, watoto na viongozi mbalimbali wa kata na vijiji wakifurahia na kushukuru kwa msaada huo.

 

 

Joram Jeremiah ambaye ni mzazi asiyejiweza kutoka kata ya Kalebezo amesema anamshukuru Mbunge Shigongo kwa kutimiza ahadi yake ambayo aliitoa kwenye kampeni kuwa atawasaidia wanachi wa Buchosa.

 

“Kweli tumeona na tumedhibitisha huyo ndiyo mbunge tuliyekuwa tunamhitaji watu wa Buchosa.

 

 

“Kiukweli wakati napewa taarifa na kiongozi wangu wa kijiji kuwa natakiwa kwenda shule na mwanangu ili nikapewe vifaa vya shule kutoka kwa Mbunge Shigongo nilishangaa kidogo.

 

 

“Lakini nilivyofika hapa shuleni tukasubiri kidogo tukaona mnakuja, ukweli nilipata furaha ambayo sikuwa nayo, nikasema moyoni kwamba mwanangu sasa anaenda shule. Mungu ambariki sana Mbunge wetu Shigongo,” alisema.

 

 

Naye  Pili Jumanne kutoka kata ya Luharanyonga amesema kwa jambo kubwa analolifanya Buchosa, amewaomba wazazi wenzake wote katika kata hiyo kuwapeleka watoto shule na kujitolea kumuunga mkono mbunge Shigongo katika kazi za maendeleo.

 

 

“Mimi kama mama mjane pamoja na kuwa sina nguvu sana lakini nitamuunga mkono Mbunge wetu Eric Shigongo katika kazi za maendeleo kwa kuwa ametufanyia jambo kubwa sana ambalo mimi pamoja na umri wangu huu sijawahi kuliona kabisa,” amesema.

 

 

 

Zoezi la ugawaji wa sare linaendelea katika kata zote 21 na vijiji vya jimbo la Buchosa kwa watoto ambapo familia zao hazina uwezo pamoja na kugawa madaftari kwa wanafunzi wote wa darasa la kwanza, shule zote za jimbo hilo ikiwa ni awamu ya kwanza kwani zoezi hili litakuwa endelevu kutokana na mahitaji kuwa makubwa kwa wanafunzi wa shule za msingi pamoja na sekondari.

 

 

 

 

Leave A Reply