The House of Favourite Newspapers

Shigongo: “Maisha Ni Magumu Sana Huko Mtaani, Magonjwa Ya Akili Yanaongezeka”-Video

0

MBUNGE wa Jimbo la Buchosha, Eric Shigongo Februari 12, 2024 amezungumza Bungeni, jijini Dodoma.

“Watanzania hawana pesa mfukoni, Watanzania hawana pesa ya kununua, watu hawawezi kuendesha maisha, wachumi watakuwa wananielewa (mimi sio mchumi) nimesoma mahali hali ya mtu kuwa na mahitaji lakini hana pesa na naliongelea kwa sababu ni Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ambayo inaratibu biashara katika Taifa letu, Mheshimiwa Mwenyekiti nikupe kwanza taswira ya hali yetu ya sasa kama Taifa, pato la Taifa linaongezeka, pato la kila mwananchi mmoja mmoja (per capital income) inaongezeka, balance of trade kati ya Tanzania na Kenya, Tanzania inauza zaidi Kenya kuliko Kenya wanavyouza Tanzania, shilingi ya Tanzania inaimarika kuliko shilingi Kenya, ni kweli zamani tulikuwa tunabadilisha shilingi ya Kenya kwa shilingi elfu 21 leo hii ni shilingi 15, ina maana shilingi yetu inaimarika licha ya uwepo wa UVIKO-19, vita vya Ukraine nk”

“Mheshimiwa Mwenyekiti hilo lipo kwenye vitabu, nikiwaeleza wananchi wa Buchosa kwamba per capital income imeongezeka, nikiwaeleza wananchi wa Buchosa kwamba GDP imeongezeka wananiambia GDP ndio nini wakat hawana kitu mfukoni, sina pesa mfukoni GDP ni kitu gani, tumeshindwa kushusha uchumi kutoka juu kwenda kwenye meza ya mwananchi wa kawaida, Mheshimiwa Mwenyekiti kwa nini tuko hapa?, tuko hapa kwa sababu ya vita nilizozitaja, tuko hapa kwa sababu ambazo awamu ya Tano (5) iliyafanya, awamu ya tano ilikuwa awamu ya kuthubutu, iliingia kwenye miradi mikubwa mikubwa ambayo si jambo baya, lakini hii maana yake ni kwamba mapato yakazidiwa na matumizi, certificate ya Bwawa ikiiva lazima Mwigulu achanganyikiwe”

“Mheshimiwa Mwenyekiti ndio hali tuliyonayo nyie wote niashahidi watu wanalalamika maisha ni magumu hawana pesa ya kununua, watu wanasitisha maisha yao kwaa sababu maisha ni magumu sana huko mtaani lakini, lakini bado magonjwa ya akili yanaongezeka, maisha yamekuwa magumu”

“Sekta za uchumi za nchi hii lazima zichangie pato la Taifa, hazichangii Mheshimiwa Mwenyekiti, agriculture (27%), tourisma imepanda kidogo, mining (10%), fishing (1.8%) Taifa letu ni tajiri mno sekta hazichangii, tunataka sekta za uchumi za nchi hii zichangie pato la Taifa ili mwisho wa siku kapu likijaa tupunguze hata kodi zetu, hakuna ubaya kapu likijaa tukasema VAT iwe 4% kwani shida nini, nikisema hivyo Wafanyabiashara wataenda kulipa kodi, faida zinaongezeka, Mheshimiwa Mwenyekiti watu hawalipi kodi, tax base yetu haifiki milioni sita (6) kwenye Taifa hili” -Buschosa ameyasema mbunge Eric Shigongo

 

Leave A Reply